Monday 7 September 2015

`Aliyemuua Alfred Kimbaa aliiba fedha

Tajiri wa mfanyabiashara wa mabegi soko kuu, jijini Arusha, Alfred Kimbaa (18), maarufu kwa jina la Mandela, aliyefariki kwa kuchinjwa hotelini na baadhi ya viungo vyake kuchukuliwa, amesema aliyefanya unyama huo  ni mtoto wa baba yake mkubwa.

Akizungumza na Nipashe, tajiri wa marehemu, Maximilian Lyatuu, mkazi wa Dar es Salaam, alisema mtoto huyo wa baba yake mkubwa alikuwa anasomea upadre.

Alisema kitendo hicho kimemuacha katika hali ngumu kutoka kwa ndugu wa marehemu, ambao hawataki kumwelea wakidhani amehusika katika kifo hicho.

Natamani ningekufa mimi huyu kijana angebaki tu hai, maana ndugu zake hawanielewi kabisa na wamenisusia msiba huu, gharama zote zangu na Rombo naenda kuzika leo (jana) sijui itakuwaje, alisema.

Lyatuu alisema chanzo cha mauaji hayo kimetokana na ndugu yake kuficha ushahidi wa wizi wa fedha alizokuwa akiiba  dukani na mara ya mwisho, Agosti 29, mwaka huu, alikwenda kulala kwa marehemu.

Alisema ilipofika saa 10 alfajiri aliamka na kuchukua ufunguo wa dukani bila mtu akimuona na kwenda kufungua duka.

Alipofika dukani alijitambulisha kwa mlinzi kuwa ni tajiri wa duka
hilo na kufungua, kisha kubeba shilingi milioni tatu na kufanya jumla ya fedha zalizoiba kufikia shilingi milioni 18,” alisema.

Alisema aliporudi nyumbani alimkuta Kimbaa (marehemu) ameamka akitafuta ufunguo wa dukani.

Lyatuu alisema, alimjibu kuwa aliuchukua kwa bahati mbaya kisha alimpa na kuondoka.

Hata hivyo, alisema Kimbaa alipokwenda dukani aligundua fedha zimechukuliwa na kuamua kumpigia simu kumuuliza.

Alisema mtuhumiwa alimwambia wakutane hotelini hapo saa 8 akiwa na matumaini ya kurudishiwa fedha lakini ikawa kinyume.

Ndugu wa marehemu, Donald Masawe,  alisema wamesikitishwa na mauaji hayo ya kinyama na kuomba jeshi hilo kuwatafuta wahusika wa tukio hilo.

Kamanda wa polisi  mkoani Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha mauaji hayo kufanyika Agosti 30, mwaka huu.

Septemba mosi, tulimkamata mtuhumiwa huyu eneo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baadaye alikwenda kutuonyesha viungo hivi, alikoficha, pembeni mwa mto Mission uliopo Usa river wilayani Arumeru,îalisema.

Alisema chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi kati yake na marehemu.
Kamanda Sabas alisema mtuhumiwa alifika Arusha, akitokea chuoni Dar es Salaam na kuishi nyumbani kwa marehemu Mianzini.

Alisema  viungo hivyo vimeunganishwa katika mwili wa marehemu na uchunguzi umefanyika juzi.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment