Monday 26 January 2015

Mwenyekiti auawa, viungo vyapikwa kama mboga

Mwenyekiti  wa Kitongoji    cha  Songambele, Kata ya Ilela Tarafa Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi, Richard Madirisha (31), ameuawa kikatili kwa kuchinjwa  shingo na kutenganishwa na kiwiliwili na kisha kunyofolewa  viungo vya mikono na miguu na sehemu za siri  na kichwa chake na viungo hivyo kupikwa ndani ya safuria kama mboga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari  mauaji hayo ya kikatili na  kutisha  yalitokea jana saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.

Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe  Meklina  Mussa na  ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na  kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.

Alisema watu hao waliodaiwa kuwa na mapanga  waliingia chumbani kwa marehemu  na kumlazisha mkewe ajifiche kwa kujifunika na shuka usoni.

 Alisema  baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu  kwa  kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu  akilia kwa uchungu.

Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawake nje ya nyumba ya marehemu.

Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu  na  kuziweka kwenye  safuria  jingine  kwenye moto   na kutokomea kusikojulikana huku  viungo hivyo vikiendelea kuchemka  ndani ya safuria hizo.

 Kidavashari alisema  mke  wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo hilo  na kukuta viongo hivyo vikiwa  ninaendelea kuchemke  kwenye safuria hizo huku kiwailiwili chake kikiwa ndani ya chumba chake

 

 Amesema uchunguzi wa  awali umebaini kuwa chanzo cha mauwaji  kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja ambae walikuwa wakiishi nae Tabora  ambae  alikuwa akimtuhumu marehemu  kuwa amemnyanya  mwanamke ambae walikuwa  na mahusiano nae ya kimapenzi ambae marehemu aliamua   kuhama nae kijijini  hapo na kuhamia nae kijiji cha Songambele  Wilaya Mlele

 

 Kamanda Kidavashari  alieleza   jeshi la polisi Mkoa wa Katavi limewakamata na linawashikilia  watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauwaji hayo ya kikatili
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment