Thursday 6 June 2013

Waziri January makamba kuburuzwa mahakamani

Chama cha Wakuluma wa Chao Usambara (Utega) kimeazimia Naibu  Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, apelekwe mahakamani kwa tuhuma za kuhamasisha wananchi kuvamia na kufanya uharibifu kwenye kiwanda cha kusindika chai cha Mponde kilichopo wilayani Lushoto mkoani Tanga.

Uamuzi wa Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli umefikiwa katika kikao cha bodi ya kiwanda hicho kilichokutana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita kujadili uasi uliofanywa kiwandani hapo.

Mwenyekiti wa chama hicho, William Shellukindo, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa Makamba atakuwa mtuhumiwa namba moja.

“Tumeazimia kumfikisha mahakama ili tupate haki yetu kwani watu hao aliowahamasisha na kuvamia kiwanda chetu si wanachama wa Utega ni wahuni na Makamba hajui historia ya kiwanda hicho amekurupuka,” alisema Shellukindo.


Alisema kitendo cha alichofanya cha kuwahamasisha wananchi kuvamia kiwanda hicho katika mkutano aliouitisha Mei 26, mwaka huu  ni ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia madaraka yake.

Shellukindo alisema kiwanda hicho ni mali ya chama hicho kwa asilimia 100 na si cha ushirika kama inavyodaiwa na kuwa licha ya kuwa na wakulima 6,000 waliokuwa wakiuza majani ya chai  wanachama halali wa Utega ni 4,000.

Alisema baada ya Utega kuchukua kiwanda hicho kutoka serikalini kilimtafuta mwekezaji baada ya wao kutokuwa na mtaji na kuwa alikuwa akikiendesha kwa kufuata taratibu.

Shellukindo alisema kufungwa kwa kiwanda hicho kila siku wanaingia hasara ya Sh. milioni 13 mbali ya mali zilizomo kiwandani, mashine kutofanya kazi na majani ya chai yaliyoharibiwa na wavamizi hao.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Chai Lushoto (Lushoto Tea Company), Nawab Mullah ambaye ni mmiliki wa kiwanda hicho, alisema mbunge huyo amewatia hasara kubwa si peke yao bali na wananchi wanaotegemea kiwanda hicho.

Mbunge wa Bumbuli, January Makamba alikiri kufanya mkutano wa wakulima wa chai jimbo lake, lakini alisema kwamba uamuzi wa kukivmia na kukifunga kiwanda hicho ulichukuliwa na wananchi  wenyewe.
chanzo:nipashe

No comments:

Post a Comment